HABARI KIBAJUNI

17 wauawa katika shambulizi la Al Shabaab


Watu 17 wameripotiwa kuuawa na wengine 20 kujeruhiwa vibaya wakati wanamgambo wa Kiislamu wa Al Shaabab waliposhambulia majengo ya wizara ya elimu mjini Mogadishu,Somalia. Mwandishi wa BBC Mohammed Moalimu,amesema kuwa wavamizi hao walilipua bomu lililotegwa ndani ya gari kwenye ukuta wa jengo hilo Kulingana na msemaji wa idara ya usalama wa ndani Mohammed Yusuf watu 8 waliuawa na wavamizi hao huku wanajeshi wawili wakipoteza maisha yao.

Askari mmoja ni wa muungano wa majeshi ya umoja wa Afrika. Msemaji huyo anasema kuwa wavamizi hao walikuwa ni 7 wawili waliojilipua langoni huku wengine watano wakikabiliwa na maafisa wa usalama. Walioshuhudia wanasema wavamizi hao walitumia bomu lililotegwa ndani ya gari kabla ya wavamizi kadhaa kuingia ndani ya jengo wakiwa wamejihami kwa bunduki za rashasha.

Msemaji wa wa kitengo cha mashambulizi cha kundi la wapiganaji wa Al Shabaab Sheikh Abdiasis Abu Musab, amethibitisha kuwa ni wao waliotekeleza shambulizi hilo na kuwa ”wapiganaji wetu wamekwisha ingia ndani ya jengo hilo lenye wizara ya elimu” Mapigano yanaendelea hadi sasa ndani ya jengo hilo baina ya majeshi ya serikali na wapiganaji hao kulingana na mwakilishi wa polisi.

Wapiganaji wa Al shabaab wametekeleza mashambulizi kama haya katika siku za hivi punde.

Mwezi uliopita wapiganaji wa Al Shabaab walishambulia hoteli moja mjini Mogadishu

Mwezi uliopita wapiganaji wa Al Shabaab walishambulia hoteli moja mjini Mogadishu uvamizi huo ulikamilika siku mbili zilizofwatia .

Waandishi wa habari walioshuhudia matukio kabla ya uvamizi huo wanadai kuwa kulikuwa na milipuko miwili mikubwa kabla ya milio ya risasi kuanza kusikika kutoka jengo hilo. hakuna kundi lililothibitisha kutekeleza shambulizi hilo lakini Al shabaan imekuwa ikitumia mbinu kama zilizotumika leo . Kundi hilo la waislamu linapinga serikali iliyoko sasa ambayo inaungwa mkono na majeshi ya Umoja wa Afrika.