HABARI KIBAJUNI

Virusi vya Corona: Idadi ya wagonjwa Kenya yafika 607 huku ikifikia Zanzibar 134


Wagonjwa hao wapya walithibitishwa hapo jana tarehe 6 mwezi 2020.

Kulingana na taarifa iliotolewa na serikali ya kisiwa hicho, Wagonjwa wote ni raia wa Tanzania, 16 wanatoka Unguja 13 wanatoka Pemba.

Wakati huohuo Kenya imetangaza wagonjwa 25 wapya wa Covid-19, na kufanya idadi ya wagonjwa nchini humo kufikia 607 tangu kisa cha kwanza cha ugonjwa huo kuripotiwa tarehe 13 Mwezi Machi.

Wizara ya afya nchini humo imesema kwamba wagonjwa 17 kati yao wanatoka Nairobi, huku eneo la Kajiado na Wajiri yakithibitisha visa viwili viwili kila moja nayo Isiolo, Mombasa na Nakuru zikiripoti kisa kimoja kimoja matawalia.

Zanzibar

Katibu mtendaji katika wizaya ya nchini Kenya Rashid Aman pia alitangaza kwamba wagonjwa saba zaidi wameachiliwa huru baada ya kupona na hivyo kufanya idadi ya waliiopona nchini humo kufikia 197.

Pia alisema kwamba wagonjwa watatu zaidi wamefariki na hivyobasi kuongeza idadi ya waliofariki nchini humo kufikia 29.