HABARI KIBAJUNI

Mabadiliko ndio kitu pekee kisichobadilika.


Abdulkadir A. Mohamed

Ulimwengu wa Leo mabadiliko ni ya haraka na ya athiri uchumi, Mila desturi na miondoko ya maisha . Kesho watoto wetu watafanya kazi vipi na kujimudu kimaisha hatuna miundo mbinu yake tayari kuwarithisha Leo .

Waliyoishi zama za waraka kusubiri majibu kwa hamu na ghamu ilhali leo majibu ni haraka alama ya rangi ya samawati kwa simu, isitoshe mtu aweza kukuona mukiwa masafa mbali sana, kuficha mema na maovo imekuwa mitihani na Hata mzuka ni mjuzi mitandaoni aweza kumjibu mtu kinyume na miaka iliyopita kumuona ilikuwa adimu Sana .

Hatuwezi kusimamisha wimbi la mabadiliko lakini ni wajibu kujifunza namna ya kupita mlangoni bila ya kuhatarisha maisha ya Leo na kesho , kusi pia watu husafiri lakini si kila nahodha husafiri wakati wa kusi na maisha ya Leo ni kusi ya kudumu.

Ni muhimu kuzingatia ya fuatayo kuishi sawia na madaliko

1. Uwezo wa kibinafsi
Ni muhimu kwa mazingira tuliyoko kila mtu kuwa na uwezo wa kiakili kwa kujifunza yanayomfa maishani mwake na kuwa na talanta kukabiliana na fikra potofu kwa kuwa na mbinu kutafautisha maslaha na shari, ulimwengu wetu shari ni biashara ya wengi waliyowema kunyamaza ndio waliyobakiwa nayo Mungu mbwahaki.

2. Ushirikiano wa wengi.
Ni lazima watu kuwa na ushirikiano kujimudu kwa mabadiliko ya Leo, Mambo ni mengi na huja kwa haraka, muhimu ushirikiano wetu kwani tunataka nyadhifa, kazi na hata ajira kukabiliana na matukio ya ulimwengu , kidole kimoja hakifunji chawa.
3. Taasisi za kijamii.
Jamii maslaha na mipangilio yake ya siku za usoni zipangiliwe na taasisi za jamii ikiwa za elimu, afya na uchumi zinachangia pakubwa kukiwa na ushirikiana na usimamizi Bora. Wasiyokuwa na viongozi hawana maadili na nguvu.

4. Uzuri hauoni kabila
Watu wachukuwe maadili mema na wajenge taswira ya maendeleo bila kujali anayeleta ni nani, hii itapunguza uhasidi na kujenga kizazi chenye fikra endelezi

5. Iitikadi salimu.
Watu wawe na itikadi sawa na wafahamu misingi ya wanayoamini sio wenye kufuata kila kipya ama kupinga kipya bila kufahamu, mabadiliko ni mengi lakini si kila badiliko lina maana na faida.

Ulimwengu ni ‘global’ hatutaishi kulinganisha maendeleo yetu na waliyokaribu nasi bali wafaa kuwa na mtazamo na mustakabali mzuri au mwema huku kujipima na walimwengu wanapoelekea, mfano Leo corona haikutoka kwetu na haikuwa shida nasi ilipoanza Lakini Leo athari yake iko milangoni mwetu Hata mtoto mdogo ajua ni hatari ilianza Uchina na Sisi tulifunzwa tutafute elimu hadi uchina kwa umbali wake Leo corona imetufunza kuwa kujitayarisha kimaisha ni lazima utafute mbinu muafaka, sio kwako tu bali ulimwengu mzima kw jumla!