HABARI KIBAJUNI

17 wauawa katika sham­bu­lizi la Al Shabaab


Watu 17 wameripotiwa ku­uawa na wengine 20 ku­jeruhiwa vibaya wakati wanamgambo wa Ki­is­lamu wa Al Shaabab wali­posham­bu­lia ma­jengo ya wiz­ara ya elimu mjini Mo­gadishu,So­ma­lia. Mwan­dishi wa BBC Mo­hammed Moal­imu,ame­sema kuwa wavamizi hao walilipua bomu lililotegwa ndani ya gari kwenye ukuta wa jengo hilo Kulin­gana na mse­maji wa idara ya us­alama wa ndani Mo­hammed Yusuf watu 8 wal­i­uawa na wavamizi hao huku wana­jeshi waw­ili wakipoteza maisha yao.

Askari mmoja ni wa muungano wa majeshi ya umoja wa Afrika. Msemaji huyo anasema kuwa wavamizi hao walikuwa ni 7 wawili waliojilipua langoni huku wengine watano wakikabiliwa na maafisa wa usalama. Walioshuhudia wanasema wavamizi hao walitumia bomu lililotegwa ndani ya gari kabla ya wavamizi kadhaa kuingia ndani ya jengo wakiwa wamejihami kwa bunduki za rashasha.

Mse­maji wa wa kitengo cha masham­bu­lizi cha kundi la wapi­ganaji wa Al Shabaab Sheikh Ab­di­a­sis Abu Musab, ame­thibitisha kuwa ni wao waliotekeleza sham­bu­lizi hilo na kuwa ”wapi­ganaji wetu wamek­wisha in­gia ndani ya jengo hilo lenye wiz­ara ya elimu” Mapigano yanaen­de­lea hadi sasa ndani ya jengo hilo baina ya ma­jeshi ya serikali na wapi­ganaji hao kulin­gana na mwak­il­ishi wa polisi.

Wapi­ganaji wa Al shabaab wame­tekeleza masham­bu­lizi kama haya katika siku za hivi punde.

Mwezi uliopita wapiganaji wa Al Shabaab walishambulia hoteli moja mjini Mogadishu

Mwezi ulio­pita wapi­ganaji wa Al Shabaab wal­isham­bu­lia hoteli moja mjini Mo­gadishu uvamizi huo ulikami­lika siku mbili zili­zofwa­tia .

Waan­dishi wa habari walioshuhu­dia matukio kabla ya uvamizi huo wanadai kuwa ku­likuwa na milipuko mi­wili mikubwa kabla ya milio ya risasi kuanza kusikika ku­toka jengo hilo. hakuna kundi lililoth­ibitisha kutekeleza sham­bu­lizi hilo lakini Al shabaan imekuwa ik­i­tu­mia mbinu kama zili­zo­tu­mika leo . Kundi hilo la wais­lamu linapinga serikali iliyoko sasa am­bayo in­aungwa mkono na ma­jeshi ya Umoja wa Afrika.