HABARI KIBAJUNI

Yemen:Serikali hupinga mad­hungu­mudho na waasi


Serikali ya Yemen iliyoko uhamis­honi, haitakubali ku­fanya mad­hungumdho ya amani na vanamgambo wa Houthi, hadi pale vanamgambo hao vatakapotekeledha maafikiano ya baradha la us­alama la umoja wa mataifa.

Mion­goni wa muafaka huo, ni kuon­doka ku­toka kachika muyi vanayoshik­ilia na kure­je­sha silaha valid­ho­tukua.

Hayo yame­semwa leo Ju­manne na makamu wa Rais Khaled Ba­hah.

Shirika la Umoya wa mataifa lilikuwa na tu­maini makubwa kuwa makundi dhote hasimu iini Yemen, kwa pamoya na kundi kuu la Houthi na serikali ya Abd-Rabbu Man­sour Hadi iliyoko uhamis­honi muyini Riyadh, yataungana kwa mad­hungu­mudho ya kuetcha amani huko Geneva ha­ti­maye mwedhi huu ili ku­jaribu kulecha su­luhu na kukome­sha mapigano dhaliy­o­dumu miedhi kad­haa sasa.