HABARI KIBAJUNI

Waan­damana kupinga ubaguzi Afrika Kusini


Maelfu ya raia wa Afrika Kusini wanaan­damana kupinga wimbi la visa vya hivi ma­juzi vya masham­bu­lizi dhidi ya raia wa ki­geni.

Miku­tano mikubwa ime­an­daliwa katika mji mkuu Jo­han­nes­burg na katika mji wa Port Eliz­a­beth ulioko kusini mwa nchi hiyo am­bao ul­ishuhu­dia masham­bu­lio kad­haa dhidi ya wa­hami­aji wa mataifa ya ki­geni mnamo mwaka 2008.

Makundi ya kiusalama yanafanya mis­ako katika ma­jumba ya makaazi katika mji wa Alexan­dra mjini Jo­han­nes­burg, ma­hala am­bapo masham­bu­lio kad­haa dhidi ya raia wa ki­geni hasa Afrika yal­i­fanyika katika kipindi cha ma­juma kad­haa yaliy­opita.

Mwaan­dishi wa BBC anasema kuwa, kuonekana kwa walinda us­alama barabarani kumeleta ud­hibiti na amani.