HABARI KIBAJUNI

Virusi vya Corona: Idadi ya wag­onjwa Kenya yafika 607 huku ik­i­fikia Zanz­ibar 134


Wag­onjwa hao wapya walithibitishwa hapo jana tarehe 6 mwezi 2020.

Kulin­gana na taar­ifa il­iotolewa na serikali ya kisiwa hi­cho, Wag­onjwa wote ni raia wa Tan­za­nia, 16 wana­toka Un­guja 13 wana­toka Pemba.

Wakati huo­huo Kenya imetangaza wag­onjwa 25 wapya wa Covid-19, na ku­fanya idadi ya wag­onjwa nchini humo ku­fikia 607 tangu kisa cha kwanza cha ugonjwa huo kuripotiwa tarehe 13 Mwezi Machi.

Wiz­ara ya afya nchini humo ime­sema kwamba wag­onjwa 17 kati yao wana­toka Nairobi, huku eneo la Ka­ji­ado na Wa­jiri yakithibitisha visa vi­wili vi­wili kila moja nayo Isi­olo, Mom­basa na Nakuru zikiripoti kisa ki­moja ki­moja matawalia.

Zanzibar

Kat­ibu mten­daji katika wiz­aya ya nchini Kenya Rashid Aman pia al­i­tangaza kwamba wag­onjwa saba zaidi wameachiliwa huru baada ya kupona na hivyo ku­fanya idadi ya wali­io­pona nchini humo ku­fikia 197.

Pia alisema kwamba wag­onjwa watatu zaidi wame­fariki na hivy­obasi kuongeza idadi ya walio­fariki nchini humo ku­fikia 29.