HABARI KIBAJUNI

Mabadi­liko ndio kitu pe­kee kisi­chobadi­lika.


Abdulkadir A. Mohamed

Ulimwengu wa Leo mabadi­liko ni ya haraka na ya athiri uchumi, Mila des­turi na mion­doko ya maisha . Kesho wa­toto wetu watafanya kazi vipi na ku­jimudu ki­maisha hatuna mi­undo mbinu yake tayari kuwarithisha Leo .

Waliy­oishi zama za waraka kusubiri ma­jibu kwa hamu na ghamu il­hali leo ma­jibu ni haraka alama ya rangi ya samawati kwa simu, isi­toshe mtu aweza kukuona mukiwa masafa mbali sana, ku­ficha mema na maovo imekuwa mi­ti­hani na Hata mzuka ni mjuzi mi­tan­daoni aweza kumjibu mtu kinyume na mi­aka iliy­opita ku­muona ilikuwa adimu Sana .

Hatuwezi kusi­mamisha wimbi la mabadi­liko lakini ni wa­jibu ku­ji­funza namna ya kupita mlan­goni bila ya kuhatar­isha maisha ya Leo na kesho , kusi pia watu husafiri lakini si kila na­hodha husafiri wakati wa kusi na maisha ya Leo ni kusi ya kudumu.

Ni muhimu kuzin­ga­tia ya fu­atayo kuishi sawia na mada­liko

1. Uwezo wa kib­i­nafsi
Ni muhimu kwa mazin­gira tuliyoko kila mtu kuwa na uwezo wa ki­ak­ili kwa ku­ji­funza yanay­omfa mais­hani mwake na kuwa na ta­lanta kuk­a­bil­iana na fikra potofu kwa kuwa na mbinu kutafautisha maslaha na shari, ulimwengu wetu shari ni bi­ashara ya wengi waliy­owema kun­ya­maza ndio waliy­obakiwa nayo Mungu mb­wa­haki.

2. Ushirikiano wa wengi.
Ni laz­ima watu kuwa na ushirikiano ku­jimudu kwa mabadi­liko ya Leo, Mambo ni mengi na huja kwa haraka, muhimu ushirikiano wetu kwani tu­nataka nyad­hifa, kazi na hata ajira kuk­a­bil­iana na matukio ya ulimwengu , ki­dole ki­moja hak­i­funji chawa.
3. Taa­sisi za ki­jamii.
Jamii maslaha na mi­pangilio yake ya siku za usoni zi­pangiliwe na taa­sisi za jamii ikiwa za elimu, afya na uchumi zi­nachangia pakubwa kukiwa na ushirikiana na usi­mamizi Bora. Wasiyokuwa na vion­gozi hawana maadili na nguvu.

4. Uzuri hauoni ka­bila
Watu wachukuwe maadili mema na wa­jenge taswira ya maen­deleo bila ku­jali anayeleta ni nani, hii ita­pun­guza uha­sidi na ku­jenga kizazi chenye fikra en­delezi

5. Iitikadi sal­imu.
Watu wawe na itikadi sawa na wafa­hamu misingi ya wanayoamini sio wenye ku­fu­ata kila kipya ama kupinga kipya bila ku­fa­hamu, mabadi­liko ni mengi lakini si kila badi­liko lina maana na faida.

Ulimwengu ni ‘glob­al’ hatu­taishi kulin­gan­isha maen­deleo yetu na waliyokaribu nasi bali wafaa kuwa na mtazamo na mus­tak­a­bali mzuri au mwema huku ku­jip­ima na wal­imwengu wanapoelekea, mfano Leo corona haiku­toka kwetu na haikuwa shida nasi ilipoanza Lakini Leo athari yake iko mi­lan­goni mwetu Hata mtoto mdogo ajua ni hatari il­ianza Uchina na Sisi tuli­fun­zwa tuta­fute elimu hadi uchina kwa um­bali wake Leo corona imetu­funza kuwa ku­ji­ta­yarisha ki­maisha ni laz­ima uta­fute mbinu muafaka, sio kwako tu bali ulimwengu mz­ima kw jumla!