CULTURE U atapo haki yako Published 8 years ago Dr Munye8y ago Namba nawe mlimwengu, pulikidha matamko Nikweledhe neno langu, udhinduwe bongo lako Nayo nda Mungu si yangu, na ayani haya yako Uatapo haki yako, utaingiya mochoni 2 Simama uchechee, usivikhofu vichuko Aliyo nayo mwendee, akupe kilicho chako Akipinga mlemee, mwandame kulla endapo Uatapo haki yako, utaingiya mochoni 3 Amkeni mulolala,na mwenye shikio koko Isive mcho kulola,nachuchidhame chwendapo Chuwate na kuduwala,usingidhi si mashiko Uatapo haki yako,utaingiya mochoni 4 Checheya kwa kula hali, usiche misukosuko Siche wingi wala mali,sabilisha roho yako Unyonge usikubali, ukaonewa kwa chako Uatapo haki yako, utaingiya mochoni 5 Siche kifaru na ndovu, wangazidi nguvu dhako Wapempe kwa uwekevu, unusuru haki yako Siandame vapumbavu,kilicho chako ni chako Uatapo haki yako, utaingiya mochoni 6 Cha mchu hakifichiki,ikafungiwa ilipo Hudhuka ikawa hiki,kadhanya utoe chako Uatapo haki yako,fahamu ni dhara kwako Leo na kwa Mola wako,utaingiya mochoni WhatsApp Facebook Twitter Email