AF-SOOMAALI

Fi­del Cas­tro afariki dunia akiwa na mi­aka 90


Fi­del Cas­tro, kion­gozi wa za­mani wa Cuba aliyeon­goza mapin­duzi ya Kiko­mu­nisti, ame­fariki dunia akiwa na umri wa mi­aka 90, kakake ametangaza.

Amiri jeshi mkuu wa mapin­duzi ya Cuba al­i­fariki dunia mwendo wa saa 22:29 usiku huu (03:29 GMT Ju­mamosi),” Rais Raul Cas­tro ametangaza.

Fi­del Cas­tro al­itawala Cuba kama taifa la chama ki­moja kwa karibu mi­aka 50 kabla ya kakake Raul kuchukua hatamu 2008.

Wa­fuasi wake walisema alikuwa ameire­je­sha Cuba kwa wananchi.

Lakini al­i­tuhu­miwa pia kwa kuwakan­damiza wap­in­zani.

Chini ya uon­gozi wa Fi­del Cas­tro, Cuba ilikuwa na uhu­siano maalum na Afrika.

Katika mi­aka ya 1970 na 80, maelfu ya madak­tari na wal­imu wa­lik­wenda Afrika na idadi sawa ya askari wa Cuba walipelekwa huko kuingilia kati mi­gogoro na wakala wa vita baridi hasa nchini An­gola.

Ak­i­toa tangazo la kifo cha kakake, Rais Cas­tro, aliyeonekana kuhuzu­nika sana, aliambia taifa kwenye tangazo la moja kwa moja kupi­tia runinga usiku kwamba Fi­del Cas­tro alikuwa ame­fariki na mwili wake uta­chomwa Ju­mamosi.

Ku­takuwa na siku kadha za maom­bolezo ya ki­taifa katika kisiwa hi­cho.

Raul Cas­tro al­i­hitimisha tangazo lake kwa ku­tamka kauli mbiu ya mapin­duzi ya Cuba: “Twaelekea kwenye ushindi, daima!”

Castro (kushoto) na Che Guevara wakati wa vita vyao dhidi ya serikaliImage copyrightGETTY IMAGES
Image captionCastro (kushoto) na Che Guevara wakati wa vita vyao dhidi ya serikali

Kando na kuandika mara kwa mara gaze­tini, Fi­del Cas­tro alikuwa ames­taafu ku­toka kwenye siasa kwa muda mrefu, mwan­dishi wa BBC Will Grant aliyepo Ha­vana anaripoti.

Mwezi Aprili, Fi­del Cas­tro al­i­toa ho­tuba nadra siku ya mwisho ya mku­tano mkuu wa Chama cha Kiko­mu­nisti.

Alikiri kwamba alikuwa amezeeka sana lakini akasema maadili ya kiko­mu­nisti kwa Cuba bado yana maana na kwamba raia “watashinda”.

“Kari­buni ni­ta­timiza mi­aka 90,” rais huyo wa za­mani alisema, na kuongeza kwamba ni “jambo am­balo sikuwahi kuli­fikiria linge­timia”.

“Hivi kari­buni, ni­takuwa kama hao wengine wote, “kwetu sote, wakati wetu laz­ima utafika””, Cas­tro alisema.

Cas­tro alik­abidhi madaraka kwa muda kwa kakake mwaka 2006 alipokuwa anau­gua maradhi ya utumbo.

Raul Cas­tro alik­abid­hiwa rasmi madaraka ya urais mi­aka mi­wili baa­daye.

Fi­del Cas­tro, Tarehe muhimu

Fidel Castro (centre) and members of his leftist guerrilla movement in Havana. Photo: January 1959Image copyrightAFP/GETTY IMAGES
  • 1926: Aza­liwa mkoa wa kaskazini mashariki wa Ori­ente nchiniCuba
  • 1953: Afungwa jela baada ya kuon­goza maasi am­bayo hayak­u­fanikiwa dhidi ya utawala wa Batista
  • 1955: Aachiliwa huru ku­toka jela chini ya mkataba wa msamaha
  • 1956: Akiwa na Che Gue­vara, aanza vita vya ku­vizia dhidi ya serikali
  • 1959: Amshinda Batista, na kuapishwa waziri mkuu wa Cuba
  • 1961: Awashinda wapi­ganaji walio­fad­hiliwa na CIA walio­vamia Bay of Pigs
  • 1962: At­i­fua mzozo wa makomb­ora wa Cuba kwa kukubali USSR iweke makomb­ora Cuba
  • 1976: Ach­ag­uliwa rais na bunge la Cuba
  • 1992: Aafikiana na Marekani kuhusu wakim­bizi wa Cuba
  • 2008: Ang’atuka madarakani kwa sababu za ki­afya