HABARI KIBAJUNI

Waandamana kupinga ubaguzi Afrika Kusini


Maelfu ya raia wa Afrika Kusini wanaandamana kupinga wimbi la visa vya hivi majuzi vya mashambulizi dhidi ya raia wa kigeni.

Mikutano mikubwa imeandaliwa katika mji mkuu Johannesburg na katika mji wa Port Elizabeth ulioko kusini mwa nchi hiyo ambao ulishuhudia mashambulio kadhaa dhidi ya wahamiaji wa mataifa ya kigeni mnamo mwaka 2008.

Makundi ya kiusalama yanafanya misako katika majumba ya makaazi katika mji wa Alexandra mjini Johannesburg, mahala ambapo mashambulio kadhaa dhidi ya raia wa kigeni hasa Afrika yalifanyika katika kipindi cha majuma kadhaa yaliyopita.

Mwaandishi wa BBC anasema kuwa, kuonekana kwa walinda usalama barabarani kumeleta udhibiti na amani.