CULTURE

U atapo haki yako


Namba nawe mlimwengu, pulikidha matamko
        Nikweledhe neno langu, udhinduwe bongo lako
        Nayo nda Mungu si yangu, na ayani haya yako
        Uatapo haki yako, utaingiya mochoni
  
                2
        Simama uchechee, usivikhofu vichuko
        Aliyo nayo mwendee, akupe kilicho chako
        Akipinga mlemee, mwandame kulla endapo
        Uatapo haki yako, utaingiya mochoni

               3
        Amkeni mulolala,na mwenye shikio koko
        Isive mcho kulola,nachuchidhame chwendapo
        Chuwate na kuduwala,usingidhi si mashiko
        Uatapo haki yako,utaingiya mochoni

               4
        Checheya kwa kula hali, usiche misukosuko
        Siche wingi wala mali,sabilisha roho yako
        Unyonge usikubali, ukaonewa kwa chako 
        Uatapo haki yako, utaingiya mochoni

               5
        Siche kifaru na ndovu, wangazidi nguvu dhako
        Wapempe kwa uwekevu, unusuru haki yako
        Siandame vapumbavu,kilicho chako ni chako
        Uatapo haki yako, utaingiya mochoni

               6
        Cha mchu hakifichiki,ikafungiwa ilipo
        Hudhuka ikawa hiki,kadhanya utoe chako
        Uatapo haki yako,fahamu ni dhara kwako
        Leo na kwa Mola wako,utaingiya mochoni