HABARI KIBAJUNI

Kipindupindu chavaua raia 15 wa Burundi


Vakimbidhi 15 va Burundi, vamefariki kutokana na ugonjwa wa kipindupindu, baada ya kukimbilia usalama vao itini Tanzania kwa mashua wakitokea iini wavo Burundi.

Hayo ni kwa mujibu wa mashirika ya vatoaji misaada.

Inasemekana kuwa vengine kadhaa vanaugua ugonjwa huo.

Shirika la Oxfam, linasema kuwa dhaidi ya vakimbidhi elfu sabini kutoka Burundi, vamefika kachika rasi moya kisiwani itini Tanzania, baada ya kutoka ghasia dha kisiasa itini Burundi.

Kwa sasa vanahamishwa kwa mashua kutoka kisiwani humo, hadi iti yavo

Kuna upungufu mkubwa wa mayi safi ya kunywa, chakula, makaadhi na huduma zdha kimatibabu.